Ben Pol Afunguka Haya Juu Ya Mipango Yake Ya Ndoa


Mwanamuziki Ben Pol anayekiki na ngoma yake ya 'Phone' amefunguka na kuweka wazi mipango yake ya ndoa na mchumba wake wa muda mrefu.

Ben kasema kwa sasa yeye kuoa bado kwani anataka kujipanga zaidi lakini pia hata ikifika wakati wa kuoa itabidi aoe kimyakimya ili kulinda 'career' yake


 Ben Pol adai ataoa kimya kimya kwani anaogopa asijekupoteza mashabiki zake kwenye muziki ambao huwa wanajipa moyo kupata nafasi hiyo.

"Mimi kuoa bado kidogo nafikiri itafika muda muafaka nitafunga ndoa, bado najipanga ila mimi naamini ndoa huwa ina tabia ya kuharibu career kidogo kwa asilimia kadhaa. Hivyo nitaoa kimya kimya kwa sababu sisi tuna mashabiki wengi na wengine wanaona huenda kukawa na nafasi kwao sasa ukioa wakajua unaweza kuwakosa hao kwenye muziki wako" alisema Ben Pol kwenye Planet Bongo ya EA Radio.
Post a Comment
Powered by Blogger.