Baada Ya Kusaini Na Roc Nation, Fat Joe Anyoosha Maelezo Sababu Ya Kuwa Chini Ya Jay ZMwezi mmoja baada ya kuwamwagisha wino The L.O.X na Yo Gotti, Jay Z ametangaza kumsaini rasmi aliyekuwa hasimu wake wa miaka ya 1990s, Fat Joe kwenye himaya ya Roc Nation. 
Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, Roc Nation wameeleza kuwa albam ya Fat Joe na Remmy Ma iliyobatizwa jina la ‘Plata o Plomo’ itakuwa ya kwanza kuachiwa chini ya label hiyo. Albam hiyo itatoka Februari 17 mwaka huu.
 
Hii imeonesha rasmi kuwa ile bifu ya miaka ya 1990s kati ya Terror Squad ya Fat Joe na Roc-Fella imepigwa chini rasmi na kugeuzwa kuwa biashara, ingawa ilianza kuonekana hivyo mwaka jana baada ya Jay Z kushiriki katika Remix ya wimbo wa Fat Joe na Remmy Ma ‘All The Way Up’.
Fat Joe amesema kuwa aliamua kuachana na bifu kati yake ya Jay Z hasa baada ya kuona Jay Z na Nas wamepiga chini bifu yao na yeye amebaki.
“Maana ya hii stori ni kwamba kulikuwa na ‘damu mbaya’ kati ya Roc-Fella na Terror Squad kwa muda mrefu na kitu kingine nilichojua niliwaona Nas na Jay Z na walikuwa katika hali ya amani. Lakini mimi nilibakizwa nje,” Fat Joe alifunguka.
Alisema kitu kilichomuingia kichwani ni kutengeneza pesa na sio bifu tena kwa hiyo mpango wa kumalizana na Jay Z ukaanzia hapo na umeishia kuwa familia ya Roc Nation.
Ni kama Fat Joe anazidisha amani ndani ya himaya ya moyo wake ikiwa ni miaka miwili tu imepita tangu walipoweka kando bifu nzito kati yake na 50 Cent.
Post a Comment
Powered by Blogger.