AY: Toka Mwaka 2006 Hakuna Rapa Amekuwa Mkubwa Zaidi Ya Joh Makini Hapa Bongo
Rapa AY ambaye hivi sasa anafanya vyema na ngoma yake 'More & More' amefunguka na kusema kuwa toka mwaka 2006 mpaka sasa hakuna rapa ambaye ameibuka na kuwa mkubwa zaidi ya Joh Makini.
AY adai kuanzia mwaka 2006 baada ya
Joh Makini kuingia kwenye kundi la 'A list' ya rapa wazuri bongo hakuna
rapa mwingine ambaye ameingia kwenye kundi hilo, ila amesema wapo rapa
wamekuwa wakijitahidi lakini wanaishia 'B, C na D list' ya rapa wakali
bongo.
"Toka mwaka 2006 hakuna rapa
amekuwa mkubwa zaidi ya Joh Makini hapa bongo, wapo wanajitahidi lakini
wengi wanaishia 'B, C na D list' hata Roma Mkatoliki ni rapa mzuri
anajitahidi, lakini natoa ushauri tu kuwa rapa tunatakiwa kuongeza nguvu
ya kujitangaza na kazi zetu, maana unaweza kuwa unaweza sana lakini
bila kujitangaza huwezi kuonekana" alisema AY kwenye Planet Bongo
Mbali na hilo AY alitoa ushauri tena kwa
wasanii wa hip hop Bongo na kuwataka kutengeneza brand zao na kazi zao
kwa kutafuta 'interview' mbalimbali na watu mbalimbali ndani na nje ya
Tanzania ili kuongeza wigo wao na kutanua mipaka ya kazi zao.
"Unajua hata rafiki yangu
Fid Q nilishawahi kumwambia hata kama wewe ni mkali na unajijua ni mkali
sana kitu kikubwa unachohitaji ni kujitangaza, hivyo rapa tunahitaji
kujitangaza sana na kutangaza kazi zetu, tujaribu kutafuta Interviews
mbalimbali, nataka kuona rapa wetu mwaka 2017 wanashiriki matamasha
makubwa, wajiongeze nina uhakika tutafanya makubwa zaidi" alisema AY