Ashley Young Yamfika Makubwa! Adaiwa Kuondoka Old Trafford Kisa Hiki


Mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini England na klabu ya Man Utd Ashley Young ameomba kuondoka Old Trafford kwa mkopo.

Gazeti la The Daily Mail limeandika kuwa, Young amefikia hatua ya kuomba kuondoka Old Trafford, baada ya kuona mambo yanaendelea kumuendea kombo tangu alipowasili meneja Jose Mourinho.

Mshambuliaji huyo ameona ni bora akaomba nafasi ya kwenda mahala pengine ili aendelee kucheza soka hata kwa mkopo.
Powered by Blogger.