Amber Lulu: Sitaki Bifu Na Mtu Mwaka Huu


Video Queen anayewika katika medani ya muziki wa kizazi kipya nchini, Amber Lulu, amesema mwaka huu hataki kujihusisha na mambo ya bifu na mastaa wenzake.

Amber Lulu amekuwa akihusishwa kuwa na bifu na video Queen mwenzake Giggy Money, ambao wote kwa nyakati tofauti wamekuwa wakishirikishwa kwenye video za wasanii wakubwa huku kambi mbili za mashabiki wao zikitumia mitandao ya kijamii kurushiana vijembe.

Staa huyo ambaye anatamba na ngoma yake ya ‘Watoma’ akimshirikisha Country Boy, amesema amekuwa akihusishwa kwenye makundi ya bifu na baadhi ya wasanii wenzake ambayo yeye hahusiki na hataki bifu na mtu.

 

“Nimekuwa nikihusishwa kuwa na bifu na marafiki zangu na wengine hata siwajui, sasa nimekuwa na sitaki tena kuhusishwa kwenye ugomvi na mtu kupitia mitandao ya kijamii,” alisema Lulu.

Mwaka 2016 Amber Lulu aliingia kwenye orodha ya Mavideo Vixen waliotupa karata zao kwenye muziki huku akidai hawezi kuiacha kazi yake ya awali na kikubwa anachoangalia ni mkwanja.
Post a Comment
Powered by Blogger.