AKA Ajipa Tuzo Yake Mwenyewe Na Hiki Hapa Alichowaahidi Mashabiki Wake.

Hakuna kitu kizuri kama mtu kufanya kitu kizuri halafu akakumbukwa na kupewa heshima, Heshima hiyo inaweza kuwa Jina lake kuwekwa kwenye vitabu vya kumbukumbu na maeneno mengine.

 Wanamuziki  na watu wengine wa sanaa hufanya kazi zao kwa weledi na baaadae hupewa tuzo ambazo hutolewa kama heshima kwao.

Hali imekua tofauti kwa Rapa AKA wa Afrika Kusini ambae ametumia mtandao wa Twitter kuziongelea mbovu tuzo za aina yeyote zile zitakazohusisha muziki wake.


Awards are played out man. They're too political. They can be bought. They depend on how nice you are to people.
The real trophy, the real award is how the people react to your music & the place you occupy in their hearts and minds.

Baada ya kuzitolea mapovu tuzo za muziki AKA pia amewaambia mashabiki wake kujiandaa na ujio wa muziki wake mzuri anaotarajia kuuachia siku za hivi karibuni.
Mbali na kuziongelea mbovu tuzo hizo pia Rapa huyo amejipa tuzo yake mwenyewe ya msanii bora wa mwaka 2017.
Post a Comment
Powered by Blogger.