AIM YA NAVYKENZO IWE SOMO KWA WABONGOFLEVA WOTE


Kundi la muziki Navykenzo linaloundwa na best Couple in Town Aika na Nahreel ndio tayari wameshaingiza sokoni albamu yao "AboveInnaMinute" (AIM).
 AIM haina muda mrefu sana lakini tayari imeanza kuchukua nafasi kubwa kwani tangu kuachiwa kwake "AIM" imeendelea kuzua gumzo mtandaoni, 

Sio mashabiki tu, hata wasanii wengine wamekua wakiizungumzia albamu hiyo.

 Mkali wa RnB RamaDee ni miongoni mwa wanamuziki walioshindwa kujizuia kuelezea mahaba waliyonayo kwenue Albamu hiyo.Ukiachana na hiyo ya Ramadee wako mashabiki kibao wanaoendelea kuisifia albamu hiyo mitandaoni kama unavyoweza kucheki na hizi post hapa chini.Kitu ambacho wanamuziki wa bongo wanatakiwa kujifunza kutoka kwa Navykenzo ni uandaaji na sio uandaaji tu, wanachotakiwa kukumbuka zaidi  ni kuwa mashabiki wanataka vitu kama hizi.
  Vitu ambavyo kwa matazamio ya kutafarika vinaweza kuishi milele pengine labda kutokana na jitihada zilizowekwa na timu iliyoshiriki ukamilishwaji wa Albamu "AIM".

Ngoma zilizomo kwenye Albamu "AIM" jumla yake ni kumi na moja ambazo Navykenzo wamewapa mashavu Alikiba, Rosa Lee, Wildad, DJ Moshe Buskila na Wanaijeria Patoranking, MrEazi na R2Bees.

Cheki  List Ya Ngoma Zote Hapa Chini:
KAMA BADO HAUJAISIKILIZA :AIM" BONYEZA HAPA KUENJOY NAYO.


Powered by Blogger.