Aika: Wasanii Wa The Industry Nao Kuja Na Album Zao


Pongezi nyingi zinazidi kutolewa na wadau wa muziki hapa Bongo kwenda kwa kundi la Navy Kenzo baada ya wakali hao kutoa album yao AIM (Above In A Minute).

Akipiga story na Dizzim Online, Aika kutoka kundi hilo ili kutaka kufahamu kama baada ya album hii na kama wana plan zozote za kutoa album nyingine.

Aika alifunguka kuwa baada ya Navy Kenzo,wasanii wengine wa The Industry ndio watakaofuata kutoa album zao pia. “Wasanii wetu wa The Industry wao ndio wanaofuata kutoa album zao,” amesema Aika.

Pia Aika alifunguka kuwa album inahitaji ubunifu wa hali ya juu na msanii huwezi kukurupuka kutoa album.


Mbali na hilo, Mashabiki wa kundi la Navy Kenzo hususan wale wa Dar wanaendelea kuifurahia album yao, Above In A Minute, wale wa nje ya Tanzania wanapaswa kusubiri kwa muda. Ni kwasababu album hiyo itaingia mtandaoni January 20.

Post a Comment
Powered by Blogger.