Aika Aweka Wazi Kinachomliza Kwa Sasa Juu Ya Album Yao 'AIM'

 aika
Zikiwa zimeshapita siku kadhaa toka kundi la Navy Kenzo waweze kuipeleka mtaani Album yao ya 'AIM' amabayo ina jumla ya ngoma 11 wasanii hao wameonyeshwa kusikitishwa na kuvunjwa moyo na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakizivujisha ngoma hizoWatu waliowanyooshea vidole zaidi ni Bloggers ambao wamekuwa wakichukua nyimbo zao kwenye Album na kuziweka kwenye mitandao ya kijamii.

Aika alisema "Kitendo cha baadhi ya watu hususani bloggers kuchukua nyimbo hizo kwenye album na kuziweka mitandaoni kinakuwa kinawavunja moyo kwani kinasababisha biashara yao kupunguza kasi na kuharibu mauzo ya album hiyo mtaani". Alisikika Akizungumza kwenye Bongo fleva Top 20 ya EA Radio

Mbali na hilo Aika alisisitiza kuwa anatambua bloggers huenda wanajua wana wa'support' kwa ku-upload nyimbo hizo kwenye mitandao ya jamii ili kusaidia album kuuzika lakini huenda wengine hawajui kile wanachofanya kinawaharibia wao soko la album yao mtaani.
Post a Comment
Powered by Blogger.