AFCON 2017: Ghana, Burkina Faso Wapata Pigo La Wachezaji Hawa


Beki wa timu ya taifa ya Ghana Baba Rahman pamoja na wachezaji wawili wa kikosi cha Burkina Faso hawatoshiriki tena michezo ya fainali za Afrika (AFCON 2017), zinazoendelea nchini Gabon, kwa sababu za kuwa majeruhi.

Mshambuliaji wa pembeni wa klabu ya Al-Nasr Jonathan Pitroipa pamoja na mwenzake wa klabu ya Almería Jonathan Zongo wameondolewa kwenye mipango ya kocha wa Burkina Faso.

Pitroipa ameumia misuli ya paja na zongo imebainika anasumbuliwa na maumivu ya goti. Kwa upande wa beki Rahman mwenye umri wa miaka 22, atakishuhudia kikosi cha Ghana kikiendelea na michezo ya AFCON akiwa nje ya uwanja, kutokana na majeraha ya goti.

Rahman kwa sasa anaitumikia klabu ya Schalke 04 kwa mopo, akitokea Chelsea ya nchini England.
Post a Comment
Powered by Blogger.