Adele: Kaeni Tayari Kwa Ndoa Yangu Mapema Mwaka HuuMkali wa muziki nchini Uingereza ambaye ametamba na wimbo wake wa ‘Hello’, Adele Adkins, amewataka mashabiki wake kusubiri ndoa yake mapema mwaka huu.

adele_two

Msanii huyo ambaye alivishwa pete tangu Oktoba mwaka jana na mpenzi wake ambaye ameishi naye kwa miaka mitano, Simon Konecki, wamepanga kufunga ndoa mwaka huu (2017).

Wawili hao walitoa tangazo mwishoni mwa mwaka jana kwamba wanatarajia kufunga ndoa Januari mwaka huu, lakini wamedai tangazo hilo limewekwa kwa muda mfupi, hivyo wamesitisha kufanyika Januari lakini wamedai itakuwa mapema mwaka huu.


Ni mwaka ambao tulikuwa tunausubiri kwa upande wangu na Konecki, tulikuwa na lengo la kufunga ndoa Januari mwaka huu, lakini tunasogeza mbele kidogo ila itakuwa mapema mwaka huu, watu wakae tayari kwa sherehe hiyo,” aliandika Adele.

Mbali na hilo, Adele anaongoza kuwa msanii tajiri zaidi nchini Uingereza kwa sasa.

Gazeti la Britain’s Heat lilitoa ripoti hiyo mnamo November 2016, kuwa kwa sasa Adele ana utajiri wa dola milioni 114 ukilinganisha na mwaka jana (2015) ambapo alikuwa na utajiri wa dola milioni 47 na kushika nafasi ya 43.

Muimbaji huyo aliongoza orodha hiyo kutokana na kuingiza fedha nyingi kutokana na mauzo kutoka kwenye albamu zake, dili za matangazo mbalimbali aliyokuwa nayo.Melody Mbassa - Nikukoleze (Official Music Video)


Post a Comment
Powered by Blogger.