Young Dee adai Ushindani unaleta uhalisia wa muziki mzuriVituo mbalimbali vya redio na TV nchini vimekuwa bize kucheza nyimbo mpya za wasanii zilizotoka kipindi cha hivi karibuni.

Utafiti mdogo nilioufanya na kubaini kuwa hawafanyi hivyo kwa mapenzi yao wala upendeleo binafsi, bali ni kuendana na kasi ya wasikilizaji na mashabiki wa kazi hizo huko mitaani ambao wamezigeuza nyimbo hizo kuwa nyimbo za taifa.


 Young Dee

Hali hii inawapa hofu baadhi ya wasanii ambao bado hawajatoa kazi au wametoa hazijawa kubwa kama zilizopo kwenye ushindani kwa sasa. Lakini hali ni tofauti kwa Rapper Young Dee.

Rapper huyo ameiambia DizzimOnline kuwa anaamini ushindani uliopo kwa sasa kwenye muziki hapa Bongo,ndio unaleta uhalisia wa muziki mzuri, kitu ambacho pengine bila ushindani tusinge kishuhudia."Kusipokuwa na ushindani ni kama kuwa darasa la kwanza halafu ushamaliza form four. Ushindani muhimu,unaongeza nguvu," amesema Young Dee.

Rapper huyo ameachia kazi yake mpya iitwayo Furaha ambayo video yake inanogeshwa na uwepo wa mpenzi wake wa siku nyingi,Tunda.
Post a Comment
Powered by Blogger.