Young Dee Adai Furaha Ni Ngoma Inayoendana Na Wakati Anaopitia


Young Dee ni moja kati ya wasanii walio achia ngoma wakati huu huku ya kwake ikijulikana kama Furaha. Hiyo ni ngoma ambayo amesema inaendana na wakati huu ambapo yeye yuko na furaha baada ya kupata mtoto wa kike.

 14262621_1655264924770976_7526476560384131072_n

Akijibu swali la Dizzim Online kuhusu kwanini ameachia Furaha wakati pia ana ngoma nyingine ambazo angeweza kuziachia pia, Young Dee amesema, “nimeiachia furaha kwa sababu ni ngoma inayoendana na hali halisi ya sasa hivi na ilikuwa ni rahisi mimi kuichagua Furaha zaidi ya ngoma nyingine kwakuwa kila ngoma ina wakati wake.”

Young Dee amefanikiwa kupata mtoto wa kike aitwaye Tamar.
Post a Comment
Powered by Blogger.