Young D atoa siri hii juu ya yule mtoto iliyodaiwa ni wa kwake, pia atoa shukrani hizi kwa Shilawadu


'Damu nzito kuliko maji' huo ni mmoja wa misemo iliyo wahi kutolewa na kuwa midomoni mwa watu hadi leo hii kutokana na uzito waneno hilo kimaana.

Lile la Young Dee kuwa na mtoto hatimae aweka wazi mkasa mzima, Katikati ya wiki hii iliyoisha ziliibuka tetesi na hadi kusambaa baadhi ya clip mbalimbali zikimuonesha mdada mmoja na mtoto iliyodaiwa kuwa ni mtu ambae aliye beba ujauzito wa rapa Young Dee.

Kupitia XXL ya CloudsFm wiki hii iliyoisha kwenye seg-ment ya U-Heard inayokuwa imeandaliwa na Soudy Brown a.k.a Mzee wa Ubuyu aliweza kumpigia sim Young Dee juu ya tuhuma hizo na Young Dee majibu yake yalikuwa hayafamu ilo jambo na huyo mtu alidai hamfahamu kabisa.

Jana kupitia ukurasa wake wa Instagram Young Dee aliweza kuweka wazi juu ya suala hilo lote na kutoa historia kwa ufupi ilikuaje mpaka kutokea kwa jambo hilo. Ujumbe wa Young D ulisomeka hivi...


Tamar (Mtoto wa Young Dee)


Nawashukuru sana watu wote ambao wamekuwa waki-support kazi yangu mpya #Furaha Either Naomba radhi kwa mashabiki zangu ambao wamekwazika kwa njia moja au nyingine kutokana na taarifa za uongo zilizosambaa mtandaoni. 

Ikumbukwe tarehe 22 June mwaka huu niliitisha press nikaomba radhi kwa waTanzania na mashabiki zangu wote kwa ujumla, nikaeleza kuwa nimepitia kipindi kigumu sana na kuwa kuna mengi nimefanya ambayo sijivunii na najutia. 

Niliahidi kubadilika na kuwa mfano mzuri kwa jamii. Kwa kipindi kirefu nimekuwa nikipigana na nafsi yangu kuhakikisha sirudii makosa. Madhara yanayotokana na matendo niliyofanya kipindi kile hadi leo bado yananitafuna ila nimekuwa nikijitahidi kukabiliana nayo. 

Nilipewa taarifa na mamisa kuwa ana mimba yangu ya (miezi 6), kama kijana nilishtuka na kupata ugumu kuikubali hali hiyo kutokana na kwamba nilikua nimetoka kwenye kipindi kigumu. Baada ya kutafakari nilimuomba aitunze hiyo mimba asiitoe!!! Kama ni mwanangu ntamlea. 

Kama ningekuwa na nia ya kumkana mtoto au kumtelekeza, kwanini nimwambie asitoe? Si kutaka kumshirikisha mtu kwanza bila kuwa na uhakika kwamba kweli mtoto ni wangu. 

screen-shot-2016-12-11-at-1-21-20-am

Management yangu sikuishirikisha kwa lolote kwa sababu inanisaidia sana katika kuhakikisha career yangu ya music ina imarika. Hivyo nilihisi ni taarifa ambayo inaweza kui-disappoint na kukatisha malengo. Hata familia yangu Mama, dada na ndugu sikuwaeleza kitu. 

Nilitaka nijipange vizuri, nijihakikishie kweli mtoto ni wangu, nitafute njia sahihi ya kueleza hili jambo. Nimesikitika sana kuona kuwa sio kila mtu anafurahia unapofanikiwa, unapoamua kufanya kazi ili upate maendeleo. 

Wapo watu ambao bado watatafuta fursa ya kukuharibia maisha. Yote kheri Namuachia mungu baba. Mtoto wangu nimempokea kwa moyo mmoja. Ni mtoto wa kike, na anaitwa Tamar. 

Nimewataarifu ndugu na wazazi wangu kuhusu hili, nashukuru wamenielewa. Nimeuelewesha pia uongozi wangu, wamenielewa. Shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa Kumjaalia uhai mwanangu, amezaliwa akiwa salama kiafya. 

Shukrani za dhati ziende kwa uongozi wangu, kwani wamekua wakihakikisha nasimama katika njia sahihi bila kuyumba. Shukrani kwenu SHILAWADU kwa kujaribu kuzirudisha nyuma jitihada zangu za kimaendeleo. #YoungDaddy

Rapper huyo baada ya tukio hilo kaamua kujipa na kujiongezea a.k.a nyingine ya Young Daddy. Mbali na hilo Young Dee ni miongoni mwa Rappers waliodondosha show ya Kibabe kwenye jukwaa la After School Bash pande za Escape one siku ya jana.
Post a Comment
Powered by Blogger.