Wema Sepetu apost haya baada ya kuumizwa tena juu ya kushindwa kuzaa Mtoto!


Kwenye mitandao ya kijamii kila siku kuna jambo, Kwake Wema Sepetu, Miss Tanzania 2006/2007 yeye maneno juu yake inaonekana hayaishi kila kukucha.Siku ya December 08, 2016, Wema amefunguka tena ya Moyoni juu ya maneno kwake kwa wale wanao mkejeli kwa kushindwa kuzaa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wema Sepetu ameandika “Did I say Gnyt…? Well maybe Not… #MyObsession @mccluretwins @mccluretwins @mccluretwins @mccluretwins … Oh and By the way, hivi mtu ukizaa haufi eeh…? Au…? Cuz I think Im missing something… Nauliza jamani…

Binaadam, Waliozaa huwa hawafi jamani…. Au…? Na wasiozaa hawafai katika jamii… Na kingine pia, Nilokosa mtoto au watoto katika Duniya hii ni mimi tu wa kuitwa Wema Sepetu au…??? Mbona mwanikalia Rohoni…. Ndio mtoto namtaka, tena Saaaana ila jamani kama Mungu kanipangia nitakuwa nae or nitakuwa nao, na kama hajanipangia pia ntasema Alhamdulillah…. Kutotoa kwa watu wengine kusiwe pigo kwangu…. Na mniwache…. Akha…!!!! alimalizia Wema
Post a Comment
Powered by Blogger.