Victoria Kimani Awatibua Tena Wakenya Kwa Kauli HiiMsanii Mrembo kutoka Kenya Victoria Kimani amesema kwasasa hana mpango wa kufanya Kolabo na Msanii yeyote yule kutoka Kenya kwa kile alichodai kuwa hakuna msanii ambae anavutiwa nae.

Image result for victoria kimani

Akihojiwa kwenye kituo cha Radio cha USIU FM cha nchini Kenya amesema “Kiukweli kuhusu wasanii wa Kenya, sidhani kuna yule ninatamani kufanya kazi naye kwa kuwa nilishamalizana nao zamani. 

Nilitamani kufanya kazi na Wyre na ikatokea, nikatamani kufanya kazi na King Kaka pia hilo likatimia ila kwa sasa sidhani kama nina picha ya msanii mwingine wa hapa ninayetamani kushirikiana naye,” Victoria Kimani alisikika akijibu moja ya swali aliloulizwa na mtangazaji.

Baada ya kauli hiyo wale watu wa Instagram na Twitter wakaanza kumjia juu kumshambulia kuwa anajidai na wengine wakamtolea ya moyoni na kumwambia hivi Album yake ya “SAFARI” nini maana yake?kwani wanaamini yeye sio mkenya ila anaigiza tu.

Victoria Kimani hii sio mara yake ya kwanza kuharibu hali ya hewa kwani Mwanzoni mwa mwaka huu pia aliwatibua wakenya kwa kuwambia hawamsapoti mrembo huyo kwenye kazi zake.

Victoria Kimani ameachia Album yake mpya ya SAFARI wiki mbili zilizo pita wapo wasanii wakubwa wengi tu kwenye Album hiyo unaweza ukainunua HAPA
Post a Comment
Powered by Blogger.