Vanessa Mdee afunguka haya kuhusu wimbo wake mpya ‘Cash Madame’


Msanii wa kike wa muziki, Vanessa Mdee amedai wazo la kuandika wimbo ‘Cash Madame’ alilipata baada ya kuzinguliwa malipo yake ya show ya promota.


Akiongea katika kipindi cha Mji Wa Burudani cha Choice FM wiki hii, Vanessa alisema “Promota alinizingua kwenye malipo hapo ndipo nilipopata wazo la kuandika wimbo wangu wa Cash Madame,”.

Pia muimbaji huyo amesema kwasasa ajipanga kufanya muziki mzuri zaidi huku akidai wakati wake wa kuwa na familia bado.

Katika hatua nyingine alisema ingawa amesomea sheria lakini kitu ambacho ameamua kukifanya katika maisha yake ni muziki.

“Ni kweli nimesomea sheria ila sijawahi kufanya kazi ya sheria na sio kwamba nilikuwa napenda sheria napenda muziki,” alisema Vanessa Mdee.
Post a Comment
Powered by Blogger.