Ujumbe Wa Kuzaliwa Wa H BABA Kwa Irene Uwoya Utakuwacha Mdomo Wazi, Soma HapaUnaweza kusema kuwa bado Mwanamuziki H baba anateseka kwa kumkosa aliyekuwa mpenzi, muigizaji Irene Uwoya, kutokana na kuendelea kumkumbuka mrembo huyo hadi katika siku yake ya kuzaliwa.

H Baba ambaye kwa sasa ni mume wa mwigizaji Flora Mvungi amemtakia kheri katika siku yake ya kuzaliwa mpenzi wake wa zamani Irene Uwoya kwa kupost picha yake Instagram na kumpa ujumbe kuwa kuachana siyo vita mpaka washindwe kutakiana kheri katika maisha yao ya kila siku.

Katika ujumbe huo H Baba amesema ukweli wa mambo yote wanaujua wao wawili na mwisho wa siku saizi kila mtu ana maisha yake na maisha yanasonga mbele"Kuachana siyo vita ya mimi nisikutakie mafanikio mema kwenye maisha yako ukweli unaujua wewe na mimi. Kikubwa tunaheshimiana, uliolewa nikaoa, una mtoto nina watoto, Una Ndiku mimi nina Mvungi wangu. Mapenzi siyo vita uwoya kazaliwa Happy Birthday Irene Uwoya 'Allah' akuongoze vyema kwenye maisha yako na mafanikio yako nakuombea baraka telee kwenye maisha yako". Aliandika H Baba
Post a Comment
Powered by Blogger.