Tunda Man: Mashabiki Hawajui Tu Diamond Ni Mtu Wangu Tangia Hata Hajawa Staa


Mkali kutoka Tip Top Connection, Tunda Man amefunguka kuhusu ukaribu wake na Diamond.

Tunda Man amejikuta kwenye mtihani baada ya mashabiki kumuandama kuhusu Cover ya wimbo wake mpya wa 'Debe Tupu'  ambayo inamuonesha Paka lakini kwenye kioo inamuonesha Simba ambayo imetafsiriwa kama dongo kwa Diamond Platnumz.

 

 “Nashindwa kuwaelewa mashabiki haya ni mambo ya u’team tu mbona Diamond na Ali wote wametokea kwenye video yangu ya Starehe Gharama si wapo mle?sasa sijui labda kwasababu wanaona sipigi picha nae ila mimi Diamond namjua hata kabla hajawa Star mimi unajua hawa wote ni watu wangu wa karibu sana“ Tunda Man alifunguka kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio.

Tunda Man kutoka Tip Top Connection na Diamond Platnumz wote wapo chini ya Menejimenti ya Babu Tale.
Post a Comment
Powered by Blogger.