Kama Unamkubali Olamide Hii IsikupiteUkihesabu haraka utagundua ni siku saba tu zimebaki kufikia Boxing Day Decemmber 26, 2016. siku amabayo Rapa mnigeria Olamide ameahidi mashabiki wake ujio wa albamu yake mpya "The Glory" .

Olamide anazo albamu zipatazo sita sokoni hivyo "The Glory" inaifanya idadi ya albamu za rapa huyo kufikia saba.

Inasemekana albamu hii itakua na kitu tofauti ambacho hajawahi kufanya kwani ngoma zote zilizo humo zitakuwa ni Hip Hop tu, Unaambiwa hakuna kuimba, hakuna kubana pua, hakuna Covers yaani ni Hip Hop mwanzo mwisho.

Sasa kama wewe ni superfan wa Olamide fanya kuusubiri mzigo uingie sokoni, Traclist hii nimeshare na wewe hapa. 

A photo posted by PèpèSneh 🌶 (@baddosneh) on


YALIYOJIRI USIKU WA EATV AWARDS: 

Post a Comment
Powered by Blogger.