Tarajia Collabo Ya AY Na Msanii Huyu Kutoka Marekani


AY ni moja ya wasanii wakongwe wenye mafanikio kunako game ya Muziki wa hapa Tanzania,mafanikio yake hayakuja hivi hivi tu bali ni kwa uchapaji kazi uliopindukia wa kuhakikisha muziki wake unakua siku hadi siku.

Mpaka sasa rapa huyo anaetamba na ngoma yake ya El-Chapo ameshafanya kolabo na wasanii wakubwa wa kimataifa kama P-Square,Sean Kingstone,Tyga,Romeo,Lamyia na wengine wengi .Habari nzuri ni kwamba huenda idadi ya wasanii wakubwa ikaongezeka, Star huyo kwani DizzimOnline wikiendi iliyopita ilipiga stori na Meneja wake ambae anasimamia kazi zake nje ya Tanzania Bwana Hemdee amesema ameshakutana na mastaa kibao nchini Marekani na huwa anaongea nao kuhusu kolabo na Ishu nyingine za Kikazi.

Mbali na hilo alidokeza pia moja ya mastaa hao ni Buster Rhymes ambae kwa mara ya kwanza alipomsikilizisha Nyimbo za AY alitokea kupenda kazi zake kwani staili ya uimbaji wake ndiyo imemvutia zaidi.

Bwana Hemdee alisema “Huwa nakutana na Wasanii wengi wakubwa Marekani na huwa nawasikilizisha nyimbo za msanii wangu (AY) naona wengi wanavutiwa na Staili ya Muziki wake ila nilifurahi sana nilipokutana na Buster Rhymes kwani aliposikiliza baadhi ya nyimbo zake alipenda sana amjue AY na hata hivyo kuna mambo tumeongea nae tutawajulisha mashabiki wetu kadri muda unavyojiri”

Kutoka Kushoto ni Hemdee ,AY na Sallam.Kutoka Kushoto ni Hemdee ,AY na Sallam

Hivyo tutarajie kolabo au kitu kingine kikubwa kwa AY kwani ni jambo la furaha pale tunapoona muziki wetu unazidi kukua siku hadi siku hata kama sio kolabo basi huenda tukamuona AY akisaini mikataba na Lebo kubwa za Muziki Duniani yote yanawezekana kwani AY profile yake ni kubwa sana.

Meneja Hemdee ambae anaishi Los Angeles nchini Marekani alikuwepo Tanzania wikiendi iliyopita na alianza  kazi ya kum”meneji AY tangia mwaka 2003,na mpaka sasa AY yupo chini ya Mameneja wawili Sallam na Hemdee.
Post a Comment
Powered by Blogger.