Tanzania imepenya! Hatiame Diana Kuietetea 'Miss world' Kesho

 
Miss Tanzania 2016 Diana Lukumay hapo kesho tar 18 Desemba 2016 anatarajiwa kuitetea Tanzania katika jukwaa la 'Miss World 2016', huku akiwa na nafasi nzuri ya kuipa matumaini Tanzania.

Mashindano hayo ambayo yanahusisha warembo zaidi ya 110 kutoka nchi mbali mbali duniani, yatafanyika katika mji wa Maryland nchini Marekani, huku mrembo wa Tanzania akifanikiwa kuingia kwenye fainali za kipengele cha 'Beauty with purpose'.


Mrembo huyo ameweza kuibua hisia za watanzania wengi kwenye mitandao ya kijamii kwa kuonyesha jitihada zake za kuitangaza Tanzania, ikiwemo kuwafundishwa lugha yKiswahili baadhi ya warembo wa nchi zingine waliofika kwenye mashindano hayo, huku akiwachezesha muziki wa Tanzania wa bongo fleva.

Mara ya mwisho ambapo Tanzania ilifutwa machozi kwenye mashindano hayo ni mwaka 2005 baada ya Miss Tanzania Nancy Sumari kushinda taji la 'Miss world Africa', na kuiwekea sifa Tanzania.

Post a Comment
Powered by Blogger.