Taarifa Ya Serikali Kuhusu Sherehe Za Uhuru Mwaka Huu

Tanzania itaadhimisha miaka 55 ya uhuru wa Tanzania Bara Desemba 9 kitaifa maadhimisho hayo yatafanyika katika uwanja wa Uhuru Dar Es Salaam.
 Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli.
Shughuli zinazotarajiwa kufanyika siku hiyo ni pamoja na:

-Gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama.
-Maonyesho ya kikosi cha makomandoo pamoja na gwaride la kimyakimya.
-Burudani za ngoma za asili za mikoa ya Mbeya, Pwani, Lindi na kimoja kutoka Zanzibar.
-Wimbo maalum ulioandaliwa na kwaya ulioandaliwa na vikosi vya Ulinzi na usalam (Polisi, Magereza, JKT na JWTZ)
-Burudani kutoka bendi ya muziki wa kizazi kipya na kizazi cha zamani.

Kauli mbiu ya sherehe za kutimiza miak 55 ya Uhuru ni "Tuunge mkono jitihada za kupinga Rushwa na ufisadi na tuimarishe uchumi wa viwanda kwa maendeleo yetu"
Kwa niaba ya Serikali natoa wito kwa wananchi wote nchini kusherehekea siku hii kwa kuwakumbuka waasisi wa nchi hii waliotetea na kutuletea uhuru.

Imetolewa Na:
Jenista .J. Mhagama (MB)
WAZIRI WA NCHI, (SERA,BUNGE,AJIRA,KAZI
VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU)
OFISI YA WAZIRI MKUU
05/12/2016
Post a Comment
Powered by Blogger.