Taarifa ya Rais wa Simba sport club kwa vingozi wa matawi yake.

simba-logo-white

Rais wa klabu ya Simba Bwana Evans Aveva atakuwa na Mkutano na viongozi wa matawi ya klabu ya Simba siku ya Jumosi ya tarehe 3-12-2016 saa Nane mchana,kwenye ukumbi wa mikutano wa klabu,uliopo barabara ya Msimbazi,hapa jijini.
Mkutano huo ni maandalizi ya Mkutano mkuu maalum wa tarehe 11-12-2016 ambao utafanyika kwenye bwalo la maafisa wa Polisi Ostrebay jijini Dar.
Pamoja na hayo,mkutano wa Rais na viongozi wa matawi,utajadili kwa kina maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu nchini, inayotarajiwa kuanza katikati ya mwezi huu.
Mwisho tuwaombe viongozi wote wa matawi kujitokeza bila ya kukosa katika mkutano huo muhimu sana kwa mustakbali wa Klabu ya Simba.
Imetolewa na; Haji S Manara
Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Sc. *SIMBA NGUVU MOJA*
Post a Comment
Powered by Blogger.