Stereo adai bila AY angeweza kuacha muziki Rapper Stereo amewahi kufanya kazi na AY kwa muda wa miaka miwili kabla ya mkataba wake kuisha.

Kutokana na na kuondoka Unity Entertainment, watu walianza kuhisi kuwa hakunufaika na chochote.

Hata hivyo akipiga story na Dizzim Online, Stereo amesema AY amemsaidia kwa mambo mengi katika kipindi wanafanya kazi na hajawahi kulalamika kuwa mambo hayakwenda sivyo.

Amedai kuwa makubaliano yao ya kazi hayakuwa kwamba ampeleke international kama wengi walivyodhani bali yalikuwa ya kusaidia kuhakikisha ngoma zake zinafika mahali.

“Bila Ambwene mimi nisingekuwa nafanya muziki mpaka sasa hivi,” amesema rapper huyo.
Post a Comment
Powered by Blogger.