Spicy Muzik: Simtumii Jaydee Kupata Umaarufu TzMsanii Spicy Muzik ambaye pia ni mpenzi wa mwanamuziki Lady Jaydee amesema hamtumii Lady Jaydee kupata umaarufu Tanzania kama inavyodaiwa na wengi, isipokuwa 'fate' ndiyo imewakutanisha. Msanii Spicy akiwa na Lady Jaydee

Akizungumza kwenye FNL ya EATV na EA Radio siku ya jana, Spicy amesema hajadate na Lady Jaydee ili kupata umaarufu, isipokuwa

“That is what it seems like, hii ni remix tuliyoifanya (akizungumzia wimbo waliotoa) nilishaachia huu wimbo nikiwa Nigeria, nature ndiyo imefanya hivi, fate ndio imefanya tuwe pamoja, sijaribu kumtumia yeyote kwa vyovyote inavyoonekana kwa mtu, najua ninachokifanya", alisema Spicy.

Pia Spicy amesema kwao wapo kimahusiano zaidi na sio kibiashara, isipokuwa kwa kuwa wapo kwenye tasnia moja sio mbaya wakifanya kazi pamoja pia.

“sisi sote ni wanamuziki na pia tuna mchanganyiko mzuri, tunaamini katika sisi zaidi tunaamini katika mapenzi na sio biashara", alisema Spicy.

Hivi karibuni wapenzi hao wameachia kazi yao mpya ambayo imekuwa gumzo kwenye mitandao baada ya wapenzi hao kuthibitisha wao ni wapenzi, kwani inafahamika Lady Jaydee sio mtu wa kuweka wazi maisha yake binafsi kwenye jamii.

  •  Cheki Darassa Alivyokinukisha Kwenye Utoaji Wa Tuzo Za EATV:

 

Post a Comment
Powered by Blogger.