Shilole Anaingiza Mkwanja Huu Kupitia Biashara Yake Ya ‘Mama Ntilie’Msanii wa Bongo Fleva Shilole ni moja ya wanawake wapambanaji sana kwenye Tasnia ya muziki wa Bongo Fleva kwani mbali na kazi zake za kimuziki lakini pia ni mjasiriamali.


Yapata Mwezi sasa umepita tangia Shilole afungue Mgahawa wake na tayari matunda yanaonekana kwani mrembo huyo kupitia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio amesema anaingiza faida ya Laki Tano Tsh 500,000/= kwa siku.


Mimi hata kama waniite mama ntilie ila najua mwisho wa siku naingiza mkwanja wangu sipungukiwi kitu nauza chakula na jioni naingiza laki tano wewe endelea tu kupiga majungu mimi napiga kazi“Amesema Shilole

Leo mrembo huyo anasheherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 28 kwa niaba ya SeetheAfricanLink tunamtakia maisha marefu na yenye Baraka.
Post a Comment
Powered by Blogger.