Scooter Braun, Meneja wa Justin Bieber na Kanye West amsaini mtoto wa David Beckham

15338423_335477703498921_4624466754473558016_n


Mtoto wa mcheza mpira wa miguu maarufu duniani, David Beckham, Cruz amesaini chini ya meneja aliyemtoa Justin Bieber.

Cruz mwenye miaka 11, ni mtoto mdogo katika watoto watatu wa kiume wa Beckham. Jumatatu hii amefungua akaunti mpya ya Instagram itakayokuwa ikisimamiwa na meneja huyo na tayari ina followers zaidi ya 134k.

Kwa mujibu wa TMZ, Scooter ni rafiki wa wazazi wake, David na Victoria, na wanaamini kuwa ni mtu sahihi wa kukuza kipaji chake. Jumatano hii, Cruz ameachia single yake ya kwanza, If Everyday Was Christmas.


 
Post a Comment
Powered by Blogger.