Romy Jons Atoa Ushauri Huu Kwa Wasanii Wasio Na Madj WaoWasanii wa Marekani na nchi nyingine duniani wamekua na utaratibu wa kuwa na Djs wao ambao wana ambatana nao kila sehemu wanapoenda kufanya show na hii inaongeza ubora na umakini kwenye performance zao.

Kwa hapa Bongo hatuna list ndefu ya wasanii wenye huo utamaduni, zaidi kwa haraka ukiuliza msanii gani anafanya hivyo wengi watamtaja Diamond Platnumz ambae ana Dj wake, Romy Jons.

Dj huyo maarufu zaidi ambae pia ni ndugu wa Diamond, ametoa ushauri kwa wasanii ambao hawana ma Dj wao hapa Bongo kama anavyofanya Diamond. Romy amesema msanii akiwa na Dj inampa urahisi kutokana na kwamba wanakuwa wamefanya mazoezi pamoja na wanakua na Chemistry nzuri zaidi.

“Mimi Diamond haniambii kwamba hapa minya watu waitikie au hapa achia watu wasiitikie.. inakuwa tayari tushajuana kwamba ikitoka nyimbo hii,inakuja nyimbo nyingine".

Pia amesema sio mbaya msanii kutokua na Dj kwani pia pesa ndogo wanazolipwa wasanii kwenye show ndio zinawafanya wasifanye baadhi ya mambo ya kimaendeleo kwenye muziki wao.
Post a Comment
Powered by Blogger.