Rich Mavoko: Kwa Mtu Anayeelewa Muziki, Hawezi Kufananisha Kokoro Na Muziki Ya Darassa


Kokoro ya Rich Mavoko na Muziki ya Darasa ni ngoma zilizotoka siku moja upande wa audio ingawa ukubwa wake wa hizi nyimbo umekua tofauti kiasi cha kuleta upinzani zaidi.

Hadi sasa mpaka naandika habari hii bado kuna watu wanazidi kuzishindanisha, ingawa mwezi December zimetoka nyimbo nyingi na hits lakini hizi zimeonekana kama kuchuana.

Nimeona sio kesi nakukusogezea maneneo ya Rich Mavoko aliyofunguka leo kwenye XXL ya Clouds Fm. Rich anasema "Kwa mtu anayeelewa muziki vizuri hawezi kufananisha zile nyimbo,zote ni hits,kwa mpango wake na kila mtu anafanya kitu chake,Darasa ni mwanamuziki mzuri uzuri ni rafiki yangu,tunafanya muziki mzuri,Nilishaisikia kabla huo wimbo,kwa sababu alietenengeneza huo wimbo ni mdogo wangu anaitwa Abaa,kuhusu kutrend youtube nani sijui kafanya nini hivyo ni vitu vya mtaani unaweza kugombana na mtu ujue kwa vitu vingine kama vya kitoto".

Darassa - Muziki
Rich Mavoko - Kokoro
Post a Comment
Powered by Blogger.