Remy Ma na Fat Joe Wataja Tarehe Ya Kutoka Kwa Album Yao 'Plata O Plomo'


Baada ya kufanya vizuri kwa wimbo wao ‘All the Way Up’, uliotajwa kuwania tuzo za Grammy mwakani, Remy Ma na Fat Joe wanatarajia kuachia album yao ya pamoja iitwayo Plata o Plomo, mwakani.

Wakali hao wa Terror Squad, wamewashirikisha wasanii mbalimbali kwenye album hiyo yenye nyimbo 12.

Nyimbo mbili zilizotoka awali, All the Way Up na Cookin zitakuwemo pia kwenye album hiyo. Wawili hao pia wameonesha kava la album yao linalowaonesha wakiwa mbele ya ikulu ya Marekani, White House.

 plata-o-plomo

Plata o Plomo inamaanisha Money or Bullets, na ni album ya kwanza wakiwa wawili. Album itaingia sokoni, Feb. 10.

Hizi ni nyimbo zitakazokuwemo kwenye album hiyo:

1. “Beast” feat. Elley

2. “Swear to God” feat. Kent Jones

3. “Spaghetti” feat. Kent Jones

4. “All The Way Up” feat. French Montana & Infrared

5. “How Can I Forget” feat. Kent Jones

6. “How Long (Interlude)”

7. “Say Yes” feat. Sevyn Streeter & BJ the Chicago Kid

8. “Heartbreak” feat. The-Dream

9. “Cookin” feat. French Montana & RySoValid

10. “Money Showers” feat. Ty Dolla $ign

11. “Too Quick” feat. Kingston

12. “Dreaming” feat. Stephanie Mills
Post a Comment
Powered by Blogger.