Prof Jay Amfungulia Darassa Njia Hii Ya Mafanikio


Msanii mkongwe wa hip hop nchini Prof. Jay amefunguka na kumtaka rapa mwenzake anayetikisa hivi sasa Darassa, asiridhike na mafanikio aliyonayo sasa bali azidi kupambana zaidi kwani huu ni mwanzo wa mafanikio makubwa yaliyoko mbele.


Prof Jay ametoa somo hilo ikiwa ni wiki ya pili toka Rapa Darassa ameachia wimbo wake mpya 'Muziki' ambao mpaka sasa umetazamwa zaidi ya mara milioni moja na laki tano kwenye mtandao wa Youtube.Prof Jay ametumia mtandao wake wa Instagram kumfikishia ujumbe Darassa na kusema alishamwambia hakuna jambo ambalo linaloshindikana chini ya jua kama akiweka mipango yake vizuri na kutimiza ndoto zake.

 "Mdogo wangu Darassa imani yako, Kutokukata tamaa na Struggle yako ya usiku na mchana ndiyo imekufanya ufikie hapo ulipofikia, nakumbuka wakati una 'shoot' wimbo wako wa usikate tamaa uliniambia unatamani ufikie level za juu kama zetu. Nami nilikwambia hakuna kinachoshindikana chini ya jua ukiseti 'goals' kufanya kazi kwa bidii na sala yote yanawezekana. 

Naamini kwa 'style' hii ya jiwe juu ya jiwe, ndoto yako inakwenda kuwa kweli, cha msingi usiridhike na mafanikio haya.. Huu ni mwanzo tuu na mafanikio makubwa zaidi yako 'at your door, Keep your eyes open and Keep ya head up' Acha maneno weka muziki" aliandika Prof Jay
Post a Comment
Powered by Blogger.