Picha: Ray C Ndani Ya Muonekano Mpya, Cheki Hapa Picha Zake

 
Unaweza kutangaza ndoa iwapo ukimuona Rehema Chalamila aka Ray C muda huu. Ni kwasababu, pole pole mrembo huyo ameanza kurejesha ule urembo wake wa mwanzo uliokuwa umepotea baada ya kutumbukia kwenye matumizi ya dawa za kulevya na kisha kuacha na kuanza kutumia dozi ya Methadone. Dozi hiyo aliyoitumia kwa takriban miaka mitatu, ilifanya anenepe na kuwa kibonge na kuwa tena si Rehema yule wa mwanzo aliyesifika kwa kiuno chake kisichokuwa na mfupa na mchezaji mahiri wa belly dance jukwaani.

Sasa Rehema karejea kwenye muonekano wake unaotamanisha macho kumtazama. Amepost picha kadhaa kwenye akaunti yake ya Instagram zikimuonesha akiwa kwenye mavazi mbalimbali ya kihindi, na hakika anapendeza.

Cheki picha hizo

Post a Comment
Powered by Blogger.