Picha: After School Bash yafana Escape One, Dar es salaam


Ile burudani iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wengi wa burudani hususani wanafunzi, namaanisha After School Bash.

After School Bash ni show inayo andaliwa na kipindi cha XXL cha CloudFm kila mwaka kwa dhumuni la kuwa kutanisha na kuwaweka pamoja wanafunzi wote kutoka shule mbalimbali kona zote za Tanzania.

Mambo yalikuwa si mambo ndani ya After School Bash pale madadaz na makakaz walipoamua kupendeza na kujisogeza pale kati, huku burudani zaikitolewa  na wasanii kama Young D, Bill Nas, Vanessa Mdee na wengine wengi.

Pia kulikuwa na kiji-segment cha kufananisha watu maarufu na wadau waliohudhuria pale na hatimae kupatikana watu watatu wakiwa wamefanana. wakwanza akiwa Jay Z, Magufuli na watatu Amber Lulu.

Pia kuna watu walifanya steji ionekane kuwa ndogo, pale walipodondosha burudani ya nguvu kiasi cha mashabiki kuingia kati na kujikuta wakizikata nyonga,.... baadhi ya nyimbo zilizotustua  watu ikiwemo ya Darassa 'Muziki', Kokoro ya Rich Mavoko na wakali wengine waliweza kutikisa vizuri nyavu pasipo na mpira.

Hizi ni baadhi ya picha juu ya show hiyoAdam Mchomvu, Jay Z (wabongo) & Mamy baby


MotokombatiVanessa Mdee


Jux


Lulu Diva


Barnaba
Post a Comment
Powered by Blogger.