Ommy Dimpoz aimwagia sifa EATV Awards


Mkali wa ngoma ya 'Kajiandae' katika anga la bongo fleva, Ommy Dimpoz amezimwagia sifa tuzo kubwa za muziki na filamu Afrika Mashariki za EATV, na kukiri kuwa mambo aliyoyaona katika shughuli ya utoaji tuzo, hajawahi kuyaona nchini Tanzania.

 

Dimpoz ambaye alitinga kwenye tuzo hizo na kupata nafasi ya ku'perform' ngoma yake ya Kajiandae akiwa na Alikiba amesema anajivunia kuona matayarisho pamoja na tuzo zenye viwango vya kimataifa na kuahidi na yeye mwakani lazima ashiriki katika tuzo hizo.

Katika hatua nyingine, Dimpoz amefunguka mbinu anazotumia kupromote kazi zake.
Post a Comment
Powered by Blogger.