Ni kazi juu ya kazi, Kanye aanza kurekodi ngoma mpya wakati bado anaendelea na matibabu

 kanye-wang


Ni kazi juu ya Kazi, huwezi kumtenganisha Kanye west na muziki, Imeripotiwa kuwa rapper huyo tayari ameanza kupika kazi mpya wakati akiendelea na matibabu.Mtandao wa TMZ umedai kuwa ameshaanza maandalizi ya album yake mpya. Vyanzo vimedai kuwa tangu arejee nyumbani amekuwa mtulivu na makini zaidi katika mambo yake.

Vimesema ametengeneza studio ya muda kwenye jumba lake la kifahari la Bel-Air ili awe na muda wa faragha anaohitaji ili apone kabisa wakati pia akitengeneza muziki mpya.

Vimesema kuwa Kanye anafananisha kilichomtokea kama ajali mbaya aliyowahi kuipata pamoja na kifo cha mama yake. Vimsema anajisikia kutengeneza nyimbo kama zile zake bora zikiwemo “Through The Wire” na ‘808s’ baada ya masahibu hayo.
 
Post a Comment
Powered by Blogger.