Nedy Music afichua sababu ya Dimpoz kumficha mpenzi wakeMsanii Nedy Music ambaye yupo chini ya label ya 'PKP' amefunguka na kuweka wazi sababu ambazo zinamfanya mwanamuziki Ommy Dimpoz na wasanii wengine Bongo kutowaweka wazi wapenzi wao kwenye mitandao ya jamii.

 

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo Nedy Music amedai mara nyingi maisha ya mapenzi ni maisha ya mtu binafsi hivyo wapo wasanii ambao hawapendi kuwaweka wapenzi wao kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa hawataki kuharibu sifa zao mbele ya jamii, na kulinda heshima zao kwa mashabiki.

"Unajua mahusiano ni mambo ambayo hayaingiliwi, hivyo isiletwe picha kuwa ni lazima unapokuwa na mwanamke au unapokuwa kwenye mahusiano lazima umposti kwenye mitando ya jamii, mimi leo kioo cha jamii nikimposti mwanamke niliyenaye kwenye mahusiano harafu kesho nikagombana naye, nikawa na mwingine tena lazima mashabiki watataka nimposti, sasa nikimfanya hivyo nitakuwa naleta picha gani kwa mashabiki na jamii kiujumla" alihoji Nedy

Nedy Music alitoa ufafanuzi huo baada ya kuulizwa kwanini bosi wake Ommy Dimpozi hajamuweka wazi mpenzi wake kwenye mitandao ya jamii kama ambavyo wasanii wengine wanavyofanya.
Post a Comment
Powered by Blogger.