Nay wa Mitego autetea uhasama wa Diamond na Alikiba, asema hayaNay wa Mitego na Diamond wamekuwa marafiki wa karibu sana kwa muda mrefu na mpaka sasa, ila ukaribu wao unaonekana kupungua kutokana na kazi mbalimbali zinazo waweka mbali.

Lakini katika hali isiyotegemewa Nay ameibuka na kuusifia muziki wa asimu wa swahiba wake Diamond, Alikiba kwa kuwa anadai ni msanii mzuri na pia akaongezea, “ ukiacha ushikaji wangu na Diamond wanachokifanya yeye na Kiba ni kitu kizuri kibiashara.”

Akipiga story na Dizzim Online, Nay amesema kuwa uhasama wao ni mzuri ila tu usifike kwenye hatua ya ugomvi wa ukweli na kutoana damu. Amesema upinzani walionao wasanii hao unafanya tasnia ya muziki ichangamke.
Post a Comment
Powered by Blogger.