Nay Wa Mitego Adai Songa Anakwenda Alipo Darassa


Rapa Nay Wa Mitego ambaye kwasasa ameachia wimbo wake 'Sijiwezi', amefunguka na kumtabiria makubwa Rapper Songa baada ya kusikia kazi yake mpya 'iitwayo 'Ni mwendo tu'.

Nay Wa Mitego alisema hayo jana alipokuwa kwenye kipindi cha Planet Bongo ya EA Radio na kuwataka wasanii wa Hip hop kubadilika na kuweka misingi pembeni ili waweze kufanya muziki wa biashara ambao unaweza kuwafanya wabadilishe maisha yao.


"Nimesikiliza na kuiona ngoma mpya ya Songa kiukweli nimeiipenda naona Songa anakwenda alipo Darassa sasa safi sana, tufanye muziki wa pesa kama hivi mambo ya misingi sijui tuiweke pembeni" alisema Nay wa Mitego 
Post a Comment
Powered by Blogger.