Nay wa Mitego Adai Ngoma Yake Ya Pale Kati Itaishi Kwa Muda Mrefu


Pamoja na baraza la sanaa la taifa, BASATA, kuufungia wimbo wa Nay wa Mitego, Pale Kati, rapper huyo amedai kuwa utaishi kwa miaka mingi. Wimbo huo ulifungiwa na BASATA mwaka huu kutokana na kuwa na ujumbe unaoendana kinyume na maadili.“Wimbo wa Pale Kati naamini ni miongoni mwa nyimbo ambazo zitaishi kwa muda mrefu kama ilivyo Nakula Ujana,” Nay ameiambia Dizzim Online.

Rapper huyo aliwahi kudai kuwa Pale Kati ilikuwa na video takribani nne tofauti lakini alifanikiwa kuitoa moja peke yake na zingine anadai kubaki nazo ndani tu.
Post a Comment
Powered by Blogger.