Mzee Baba Akamatwa Uwanja Wa Ndege Akitoroka Kesi Ya Kutishia Kumuua Mama Yake

Farid Juma  Janmohammed lakini yeye hupenda kujiita Fuad Jamal a.k.a Mzee Baba amekamatwa  uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akisubiri Kupanda ndege ya  kuelekea uingereza Huku akijua fika kuwa ana kesi ya kutishia kumuua mama yake mzazi,
Chanzo chetu kimedai kuwa "alipoona hukumu inakaribia machale yakamcheza akaona bora akimbie "  Kilisema Chanzo chetu.

Mpaka wakati huu Inasemekana Mzee Baba yupo Polisi Kwa ajili ya mahojiano na alipojaribu kuomba dhamana ilishindikana kutokana na Mtuhumiwa huyo kumiliki Passport mbili Za kusafiria moja ikimtambulisha Kama raia wa uingereza na nyingine ikimtambulisha Kama Raia wa Tanzania

MGOGORO NA MAMA YAKE:


Inadaiwa kuwa chanzo cha mgogoro Kati ya mtu na mamaake ni masuala ya Nyumba,
 Nyumba ambayo mama yake aliingia mkataba Na mwekezaji fulani jina kapuni, kwamba Nyumba aliyokuwa anaimiliki ivunjwe Na kujengwa Ghorofa ambalo chini kuna frames halafu juu kuna makazi ya watu, mchongo ukafanyika Mama akapewa baadhi ya Vyumba kwa makubaliano kwamba baada ya Miaka kadhaa Atamiliki Ghorofa lake lote mwenyewe, basi mama akaamua kuwakabidhi wanae Funguo moja moja,
sasa inasemekana Farid akaingiwa na tamaa na kutaka apendelewe zaidi Kwa kupewa nyumba zaidi ya moja ndani ya Ghorofa Hilo, hivyo  akawa anamlazimisha mama yake Kwa kutishia kumuua kitu ambacho mama yake alikipinga, Ndipo Jamaa huyo akawa anamtishia kumuua na hii si Mara ya kwanza Siku ya Siku Farid alimvamia mama yake akiwa na kundi la wahuni inasemekana kuwa Walitishia kumuua Mama Kama akienda kinyume na makubaliano Yao,

 Bahati Nzuri majirani na baadhi ya Ndugu waliskia  makelele ikabidi wakaingilie Kati na kwenda kumuokoa mama yao,  mtuhumiwa na wenzake wakachoropoka ikabidi mama akatoe ripoti Polisi ikafunguliwa kesi na kuanza kuunguruma Ndipo Farid alipoona maji yanamfika shingoni Akaona bora atoroke nchi,  Polisi walipopata taarifa ndo wakamkamata uwanja wa Ndege na kumuuweka chini ya ulinzi.


BILNAS X T.I.D - LIGI NDOGO (FIESTA DAR 2016) 

Post a Comment
Powered by Blogger.