Mwasiti Ataja Sifa Hizi 4 Za Mwanaume Ambaye Anahitaji Kuwa Naye


Mwanamuziki Mwasiti ambaye anafanya vizuri na wimbo wake 'Kaa nao' amefunguka na kuweka hadharani sifa za mwanaume ambaye anahitaji kuwa naye katika maisha yake na kusema haiwezekani hata siku moja mtu na mpenzi wake wakawasiliana mara moja kwa siku.

 Mwasiti amesema kuwa angependa mume wake kwanza awe mcha Mungu na mwelewa ili wapendane na kujaliana kweli ila yote hayo yabebwe na msingi mkuu wa mapenzi ambao ni mawasiliano mazuri kati yao.

"Mwanaume wangu mimi awe anampenda sana Mungu kwani mimi naheshimu sana dini yangu,  hivyo napenda mume wangu awe mcha Mungu mwelewaji, understanding, caring, loving and sharing hivi vinne ndiyo muhimu. Tupendane, tugawane, tuelewane na tufanye mawasiliano kwa sababu wewe huwezi kuwa boyfriend harafu siku nzima usiku tu ndiyo unatoka na ujumbe wa simu eti 'good night' hata kama mtu yupo busy lakini hakuna ubusy wa namna hiyo kwa waubani" alisikika Mwasiti kwenye Planet Bongo.
Post a Comment
Powered by Blogger.