Mwana FA aweka rekodi hii Youtube kupitia ngoma yake mpya 'Dume Suruali'


Ni ukweli kuwa muziki wa Hip Hop unaanza kupata heshima yake nchini. Baada ya kuonekana utofauti wa muziki wa Mwana FA kwenye nyimbo zake za hivi karibuni, rapper huyo anaanza kusherehekea baada ya video ya wimbo wake mpya kuanza kujitengenezea rekodi zake binafsi.

 15276700_1774378012779920_5374757292946227200_n

Mwana FA

Video ya wimbo wake mpya ‘Dume Suruali’ aliomshirikisha Vanessa Mdee umefanikiwa kutazamwa zaidi ya mara milioni moja ndani ya wiki mbili kwenye mtandao wa Youtube. Nao wimbo wa Darassa ‘Muziki’ umefanya hivyo siku chache zilizopita.


Post a Comment
Powered by Blogger.