Mwana FA afunguka ushindi wa Bony Love Eatv Awards


Msanii Mwana FA ambaye alikuwa kwenye kinyang'anyiro cha kipengele cha mwanamuziki bora wa kiume kwenye EATV Awards, ametoa pongezi kwa tuzo hizo, kwa kitendo cha kutoa tuzo ya heshima kwa Dj Bonny Love.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram Mwana FA amefurahia ushindi wa Dj Bonny Love huku akikumbushia historia ya maisha yake kimuziki, na kwamba bila Dj huyo asingefika hapa alipo sasa.

Ujumbe wa FA ulisomeka hivi..

 

Sidhani kama ningefanya mziki kama sio Boni..brother ndio alikuwa mtu wa kwanza kwenye industry kuniamini na kunipa nafasi..i cant thank you enough mzazi,EVER..nimefarijika mno..asante sana EATV kwa kumpa tuzo ya heshima,ambayo ni stahili yake @boniluv ..hongera sana mzazi! Pia hongera nyingi kwa EATV kwa kufanikisha hili zoezi la tuzo..hongereni kwa hii platform na kiukweli haikukaa kama ndio mara ya kwanza kwa jinsi mlivyoipatia..hatua kuelekea kwenye right direction,MMETISHA SANA..

Pia Mwana FA amesema kufanyika kwa tuzo hizo ni mwanzo wa kuelekeo kuzuri zaidi kwenye sanaa ya Tanzania.

 

BJ Bonny Love akipokea tuzo ya heshima aliyokabidhiwa na Waziri Nape Nnauye
Post a Comment
Powered by Blogger.