Mr T Touch: Darassa amebadilika mwenyewe sijambadilishaDarasa alitoka kwa njia ya Hip Hop ya kiharakati, ngumu sana. Lakini sasa rapper huyo ameweza kubadilika kutoka kwenye Hip Hop ngumu ya harakati hadi kwenye Hip Hop ya kuchezeka, na amefanikiwa.


 Darassa

Watu wengi wamekuwa wakiamini kuwa mtayarishaji wa muziki anayefanya naye kazi kwa sasa, Mr T Touch ndiYe amembadilisha.

Akipiga story na Dizzim Online, Mr T amesema Darassa ameamua kubadilika mwenyewe. Rapper huyo anafanya vizuri kwa sasa na wimbo wake Muziki ambao kwa wiki mbili video yake imepata views milioni 1 kwenye mtandao wa Youtube.
Post a Comment
Powered by Blogger.