Meneja Wa Chuchu Hansy Ataja Sababu Ya Kupanda Stejini Na Taulo

Hamisi Mbega ambaye ni meneja wa msanii wa filamu Chuchu Hansy aliyeibuka na ushindi wa muigizaji bora wa kike kwenye EATV AWARDS iliyofanyika Disemba hii, amesema yeye ana akili timamu hivyo kuvaa taulo kwenye usiku wa tuzo watu wasimuelewe tofauti.

Bw. Mbega ambaye ni meneja wa ChuChu Hansy akifanya mahojiano na Sam Missago wa EATV

Akizungumza na EATV meneja huyo aliyeacha mshangao kwa mashabiki waliokuja kushuhudia tukio hilo kubwa kwenye tasnia ya sanaa hapa nchini, amesema aliamua kuvaa hivyo ili kuleta otofauti na wengine waliohudhuria, kwani taulo pia ni nguo kama nguo zingine.

“Taulo ni nguo, mi nashangaa sana watu wanavyokuwa wamekengeuka kuona mtu amevaa taulo, labda angevaa meneja wa R Kelly au Jay Z ingeonekana ni kawaida, lakini amevaa mtanzania inakuwa ni tatizo, mi nimevaa kwa sababu nimeangalia ni jinsi gani naweza kutoka tofauti, wengi wamenifikiria labda jamaa na upungufu wa akili lakini ukweli ni kwamba nina akili kuliko hata hao wenye akili”, alisema Bw. Mbega.

Mbega aliendelea kusema kuwa alijaribu nguo kadhaa lakini hazikumvutia, hivyo akaona ni bora achukue taulo.

“Wenzangu walioingia pale, walikuwa watu wana masuti na vitu kibao, nikaesma na mimi nikivaa suti nitakuwa kama naenda kwenye kipaimara mwili mdogo ngoja nivae taulo na kweli limeleta utofauti”, alisema Mbega.
Post a Comment
Powered by Blogger.