Mahakama Nchini Uganda Yaamuru Wizkid Kukamatwa

 
Msanii Wizkid kutoka Nigeria huenda akatupwa jera baada ya kuahirisha Tamasha alilopangiwa kuperform Desemba 3 mwaka huu nchini Uganda na yeye kutoa taarifa kuwa hatakuwepo bila kutoa taarifa za kiundani za kutokuhudhuria kwake wala Menejimenti yake kufikisha taarifa mapema .

Mahakama ya  Buganda Road Nchini Uganda Ijumaa iliyopita imeamuru kukamatwa kwa Wizkid popote pale alipo na polisi wa Kimataifa (Interpol) baada ya kutokufika kwenye Tamasha hilo ile hali alikua tayari ameshalipwa mkwanja wake.


 

Kwa mujibu wa Mwanasheria wa Face Tv ambao hao ndiyo waliandaa Tamasha hilo Bw.Fred Muwema amesema Wizkid alilipwa kiasi cha Dola $60,000 kupitia kwa Meneja wake Sunday lakini kwasababu zisizowekwa wazi hakufika kwenye Tamasha.

Zaidi ya watu 25,000 walikuwa tayari wamelipia Tiketi za Tamasha hilo ambalo hata hivyo mwanasheria huyo amedai wameingia hasara ya zaidi ya Dola $300,000 kwa uzembe wa Menejimenti ya Wizkid kwani mpaka Dakika za mwisho hakukuwa na Taarifa yoyote ya kutokufika kwa  starboy huyo Wizkid.
Post a Comment
Powered by Blogger.