Lulu Diva: Nilitaka Kufanya Kazi Na Mwanamuziki Sio Muimbaji Ndiyo Maana Nikamshirikisha Barnaba
Modo wa Video na Msanii Chipukizi wa Muziki Lulu Diva, amesema kwake Barnaba ni Mwanamuziki aliyekamilika katika nyanja zote na Ndio maana akamshirikisha katika wimbo wake uitwao ‘Milele’.

Lulu Diva: Nilitaka kufanya kazi na Mwanamuziki sio Muimbaji ndiyo maana nikamshirikisha Barnaba.

Akiongea kupitia kipindi cha The Playlist cha Times Fm Jumamosi iliyopita, Lulu Diva amedai kuwa Wasanii wengi ni Waimbaji na si Wanamuziki waliokamilika kama ilivyo kwa Barnaba.

“Nilitaka kufanya kazi na Mwanamuziki sio Muimbaji ndiyo maana nikamshirikisha Barnaba, namuelewa sana ni msanii aliyekamilika” Alisema Lulu Diva.

Katika hatua nyingine Lulu Diva amedai kuwa video ya wimbo wake huo ‘Milele’ aliyoirekodi nchini Afrika Kusini imetumia zaidi ya Milioni 40.


Lulu Diva ft Barnaba - Milele (Official Video) 

Post a Comment
Powered by Blogger.