Lile la Lord Eyes Kusainishwa na Barakah The Prince, Hatimae Bonta Afunguka Haya

 
Rapper Bonta amedai kuwa kusainishwa kwa Lord Eyez kwa ile iliyodaiwa kuwa ni label mpya ya Barakah The Prince, ni aibu kubwa kwenye jamii ya hip hop.

 Bonta akiwa na Lord Eyez

Akipiga story na tovuti ya Bongo5, Bonta alisema  “Kama ni kweli imetokea basi ni AIBU kubwa sana kwa game ya hiphop,”

“Ni ngumu sisi kusimama mbele za watu na kujinadi kuwa we are hiphop. Other way round ni hasara kwa Barakah sababu unaweza kukuta amemsaini MONSTER ambaye atarule out game yake. 

Angetakiwa kujiuliza huyu mtu kama kashindwana na watu wake aliogrow nao itakuwa mimi ambae yeye alikuwa role modelwangu?” amehoji rapper huyo ambaye naye ni member wa Weusi.

Kwa jicho la 3 pia Barakah ni kati ya wasanii wachache Tanzania waliofanikiwa kuiangusha hip hop. Na vijana pia tujifunze kuhusu kuanguka mapema kwa watu kama Chuji, Boban, Chid, Lord, Fanani etc.

No matter kipaji kiasi gani ila wewe mwenyewe unaweza kukiharibu kwa external things/forces utakazotumia.

Kupitia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, jana Barakah alitangaza kuanzisha label yake iitwayo Bana, ambayo kwa kuanzia itamsimamia Lord Eyez, Naj na msanii mwingine.

-Bongo5
Post a Comment
Powered by Blogger.