Ligi Kuu England: Arsenal Walala 2-1 Mbele Ya Everton

 Arsenal walishinda michezo mitatu kabla ya kufungwa na Everton
Arsenal wamepoteza nafasi ya kukaa kileleni mwa ligi kuu ya England baada ya Everton kutoka nyuma na kuondoka na ushindi wa 2-1.

Washika bunduki hao walishinda michezo mitatu mfululizo walianza vyema katika mchezo dhidi ya Everton baada ya Alexis Sanchez kupiga safi mkwaju wa adhabu nje kidogo ya eneo la hatari uliombabatiza mlinzi Ashley Williams na kuingia wavuni.

Arsenal walishinda michezo mitatu kabla ya kufungwa na EvertonArsenal walishinda michezo mitatu kabla ya kufungwa na Everton

Everton walisawazisha na kuwa dakika chache kabla ya kwenda mapumzikoni baada ya Seamus Coleman kumalizia vyema mpira uliopigwa na mlinzi Leighton Baines.

Kipindi cha pili kila timu ilirejea kwa lengo la kuchukua alama tatu lakini ni Everton ndio waliofanikiwa baada ya Williams kufuta makosa yake kwa kuifungia Everton goli la pili na la ushindi.

Idrissa Gueye aling'ara katika mchezo huo kwa kupiga pasi 51Idrissa Gueye aling'ara katika mchezo huo kwa kupiga pasi 51

Kwa matokeo hayo Arsenal wanabaki nafasi ya pili wakiwa na alama 34 wakiwa mbele kwa mchezo mmoja dhidi ya vinara Chelsea wenye alama 37.

Everton wanabakia nafasi ya saba wakiwa na alama 23.

Nahodha wa timu ya Everton Phil Jagielka alitolewa kwa kadi nyekundu dakika chache tu kabla ya kumalizika kwa mchezo huo baada kupata kadi ya pili ya njano.
Post a Comment
Powered by Blogger.